Genesis 26:15-20

15Kwa hiyo visima vyote vilivyochimbwa na watumishi wakati wa Ibrahimu baba yake, Wafilisti wakavifukia, wakavijaza udongo.

16Ndipo Abimeleki akamwambia Isaka, “Ondoka kwetu, kwa maana umetuzidi nguvu sana.”

17Basi Isaka akatoka huko akajenga kambi katika Bonde la Gerari, akaishi huko. 18Ndipo Isaka akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Ibrahimu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Ibrahimu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa.

19Watumishi wa Isaka wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi. 20Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki,
Eseki maana yake ni Ugomvi.
kwa sababu waligombana naye.
Copyright information for SwhKC